Tarehe 18 mpaka 24 mwezi huu wa Novemba ni wiki ya uhamasishaji wa matumizi sahihi ya dawa za kutibu maambukizi ya bakteria ama Antibiotics, na sababu zinazoweza kusababisha usugu wa bakteria dhidi ya dawa hizo. Lilian Mtono anazungumza na Rais wa Chama cha Mafamasia huko Tanzania, Fadhili Hezekiah kuhusiana na suala hili na kwanza alihoji, lipi kubwa kwenye maadhimisho haya?