1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Zanzibar na katiba ya Jamhuri ya Muungano

13 Juni 2012

Leo tarehe13.06.2012, baraza la Wawakilishi Zanzibar limepokea Sheria Nambari 8 ya mwaka 2012 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

https://p.dw.com/p/15DBk
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho KikwetePicha: AP Photo

Sheria hiyo imewekwa sahihi na Rais Kikwete juu ya kuanzishwa kwa tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Wananchi kuelekea uandishi wa Katiba Mpya.

Lakini kama katiba ya Zanzibar inavyosemwa ni kwamba sheria hiyo iwasilishwe tu kwa taarifa na wala isijadiliwe katika baraza la wawakilishi visiwani humo. Hamza Hassan ni mwakilishi wa baraza hilo na anasema kuna vipengee vingi katika katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania ambavyo vinapaswa kubadilishwa ili kuwpa nguvu ya kuamua maswala fulani yanayohusu mustakbal wa nchi.

Amina Abubakar amezungumza naye na mwanzo anatupa maoni yake juu ya kuwasilishwa kwa sheria hii.

(Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi Amina Abubakar

Mhariri Othman Miraji