Tanzania inawakumbuka mashujaa wa Vita vya Maji Maji dhidi ya ukoloni wa Ujerumani kati ya Julai 1905 – Julai 1907, wakati taifa hilo lilipokuwa likijulikana kama Tanganyika. Chimbuko la vita hivyo ni kijiji cha Nandete, Mkoa wa Lindi na viliongozwa na Kinjeketile Ngwale aliyewaaminisha wenzake kuwa maji yanaweza kuzuia risasi. Watu 250,000–300,000 walipoteza maisha.