Tanzania yapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa
27 Novemba 2024Karibu Watanzania milioni 31 wamesajiliwa kupiga kura kuwachagua viongozi wa mitaa na vijiji ambao wana nguvu katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Mamia ya wapiga kura walipanga mistari kote nchini humo kabla ya hata vituo vya kupigia kura kufunguliwa rasmi. Chama tawala CCM cha Rais Samia Suluhu Hassan, ambacho kimekuwa na nguvu kwa miongo mingi, kinakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa upinzani uliosusia uchaguzi huo mwaka wa 2019 kikitaja ghasia na kutishwa. Wasiwasi wa aina hiyo umeugubika uchaguzi wa mwaka huu huku chama kikuu cha upinzani Chadema kikisema wagombea wake wengi walienguliwa isivyo halali kwenye mchuano huo. Rais Samia ameondoa hofu hiyo akiahidi kinyang'anyiro hicho kitakuwa cha haki. Ni mtihani wa kwanza kwenye uchaguzi kwa Rais Samia tangu alipochukua usukani baada ya kifo cha ghafla cha mtangulizi wake John Magufuli mwaka wa 2021.