1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yaonya wageni juu tahadhari za usalama

30 Januari 2023

Serikali ya Tanzania imewataka wadau wa Maendeleo kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni kuacha kutoa taarifa kuhusiana na hali ya usalama nchini humo bila kuishirikisha serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki

https://p.dw.com/p/4MsbU
Stergomena Tax SADC
Picha: Valery Sharifulin/TAS/dpa/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje Tanzania imetoa kauli  hiyo ikiwa ni siku chache tangu ubalozi wa Marekani nchini humo kuonya wananchi wake juu ya viashiria vya matishio la kigaini mjini Dar es salaam.

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika mji mkuu wa taifa hilo la Afrika Mashariki Dodoma,Waziri mwenye dhamana Stagomena Taxi, alisema kuna taratibu katika kutoa taarifa.

Alisemausalama wa nchi zote ni jukumu la nchi husikakwa hivyo hilo ni jukumu la serikali, hivyo yeyote mwenye taarifa anapaswa kushirikiana na mamalaka inayohusika.

"Sio peke yako unaamua tu kutoa matamko, hapana, pengine ameona viashiria."

Alisema kutokana na mashirikiano baina ya mataifa husika ndio maana wizara kwa ujumla wake inasisitiza mawasiliano rasmi pande husika.

Soma zaidi:Tanzania yataka ulinzi imara katika mpaka wake na Burundi

Aidha wizara hiyo ya mambo ya nje na mashirikiano ya Afrika mashariki, ilisema inaendelea kushirikiana vema na washirika wake wa maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Polisi yawatoa wasiwasi raia

Baada ya taarifa ya Ubalozi wa Marekani juu ya kuwepo kwa viashiria vya matukio ya kigaidikusambaa katika mitandao ya kijamii, kulizusha taharuki katika jiji kuu la kiuchumi Dar es salaam.

Tanzania yaondoa hofu ya fununu za shambulizi Dar es Salaam

Jeshi la polisi nchini humo limewatoa wasiwasi wakaazi katika mkoa huo wenye shughuli nyingi za kiuchumi na kuahidi kuimarisha hali ya usalama.

Akizungumza siku na vyombo vya habari, Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime amewahakikishia wananchi usalama wao na kuwataka kuwa waangalifu.

"Jeshi la Polisi Tanzania tulianza kulifanyia kazi taarifa hiyo kwa kina toka iliponza kusambaa."

Aliwatolea wito raia endapo kuna jambo la kutilia shaka wasisite kutoa taarifa, kwani hakuna taarifa inayopuuziwa linapokuja suala la usalama wa watu na mali.

Soma zaidi:Polisi Tanzania yadai muuaji wa maafisa usalama alikuwa gaidi

"Aidha pale itakapobainika jambo lenye kutia shaka au mtu/watu wenye kutia mashaka taarifa hizo ziripotiwe kwa haraka ili ziweze kufanyiwa kazi”

Safari za ndege za sitishwa kutokana na kitisho

Juma lililopita Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulitoa taarifa ikiwaonya raia wake, ju ya makundi ya kigaidi yanaweza kushambulia kwa tahadhari kidogo au bila kutoa tahadahri.

Symbolbild Flugverkehr
Ndege za shirika la ndege la Uholanzi KLM zikiwa kwenye maegeshoPicha: Remko De Waal/AFP

Taarifa hiyo ilionya juu ya maeneo ambayo yangelengwa ni pamoja na  hoteli, balozi, migahawa, maduka makubwa na soko, vituo vya polisi, maeneo ya ibada na maeneo mengine ambayo wanayatembelea.

Kutokana na taarifa hizo baadhi ya mashirika ya ndege ikiwemo Shirika la ndege la uholanzi KLM lilisitisha safari zake nchini Tanzania.

Nchi zilizoko katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, zilikumbwa na tukio la mashambulizi mawili ya kigaidi yaliyotekelezwa kwa wakati mmoja.

Soma zaidi:Serikali ya Tanzania yatoa ripoti ya ajali ya ndege

mashambulizi hayo yalizilenga balozi za Marekani zilizopo katika Miji ya Nairobi nchini Kenya na Dar Es Salaam Tanzania.

Mashambulizi hayo ya Agosti mwaka wa 1998,yalibadilisha hali ya usalama wa ukanda wa Afrika Mashariki na kuzitosa nchi hizo katika kampeni iliyojulikana kama vita vya kimataifa dhidi ya ugaidi.