Serikali ya Tanzania imeyashutumu baadhi ya mashirika ya kimataifa kwa kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu mpango wa kuwarejesha wakimbizi wa Burundi. Hivi karibuni baadhi ya ripoti zilidai kuwa serikali ya Tanzania imekuwa ikiwashurutisha wakimbizi hao kurejea makwao jambo ambalo lilielezwa kuwa ni kinyume na makubaliano ya pande tatu yaliyofikiwa miaka ya hivi karibuni. George Njogopa anaripoti.