Tanzania imeipatia Uturuki dola milioni 1 ya msaada wa kibinadamu kufuatia taifa hilo kukumbwa na janga la tetemeko la ardhi lilitokea hivi karibuni. Hatua hiyo imeibua mjadala mkubwa katika jamii huku baadhi wakionekana kupongeza lakini wengi wanahoji wakisema msaada huo unatolewa wakati maeneo mengi ya nchi yanakabiliwa na hali ngumu, kama vile uchakavu wa mashule, hospitali na mfumuko wa bei.