Benki ya Dunia imetangaza rasmi Tanzania imeingia katika uchumi wa kipato cha kati ngazi ya chini kuanzia Julai mosi tarehe ya kwanza ya mwaka wake mpya wa fedha, na hivyo kujiunga na mataifa saba ya eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa dira yake ya maendeleo Tanzania ilipanga kuingia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.