Kuelekea uchaguzi mkuu Jumatano nchini Tanzania, baadhi ya wapiga kura wanasema taarifa zao katika vituo vya kipigia kura zimekosewa. Kuna wanaosema wamekosewa umri na wengine wameandikwa kuwa sio watu wazima hali ambayo inaleta ukakasi juu ya iwapo ni uzima wa umri au uzima wa uhai.