1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania kuweka vituo vya udhibiti Ebola

28 Septemba 2022

Wizara ya afya nchini Tanzania leo imetangaza mikakati ya kujiweka tayari kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ikiwamo kuimarisha udhibiti katika maeneo ya mipakani baada ya Uganda kutangaza mlipuko huo wiki iliopita

https://p.dw.com/p/4HTci
Uganda Ausbruch von Ebola
Picha: BADRU KATUMBA/AFP via Getty Images

Hadi sasa taifa hilo la Afrika Mashariki halidhibitisha kisa chochote ya mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa huo, ambao hivi karibuni umeripotiwa kuwepo nchini jirani ya Uganda.

Waziri wa afya, ummy mwalimu amewaagiza waganga wakuu wa mikoa kote nchini kutenga vituo maalumu vitakavyotoa huduma za haraka kwa wanachi wanaohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Mikoa ambayo inapakana na mataifa ambayo tayari yamewahi kushuhudia visa vya maambukizi hayo ikiamriwa kuchukua hatua mujarabu kuhakikisha huduma inakuwepo kwa muda wote.

Amesema licha kwamba hakuna kisa cha kuwepo kwa mgonjwa yoyote, lakini hiyo haimanishi serikali kutochukua hatua za kujilinda na kwa maana hiyo hatua zote zitazosaidia kujiweka kando na maambukizi

Soma Pia:Kenya yajiweka sawa dhidi ya Ebola

"Nawaagiza wakuu wa mikoa kote nchini kila mkoa kujiandaa" Alisema waziri ummy katika mkutano wake na waandishi wa habari na kuongeza kwamba kila idara inatakiwa kujiweka tayari.

Aidha amezitaka mamalaka za mikoa kutodharau aina yoyote ya tetesi kuhusiana na washukiwa wa homa hiyo na kuhakikisha eneo la mazishi linatengwa.

"Tukipata kifo cha mgonjwa wa Ebola leo tunapaswa kujua tutamuhifadhi wapi." Aliongeza waziri huyo wa afya na kusisitiza kwamba kila washukiwa wanapaswa kutengwa kulingana na maelekezo ya wataalamu wa masuala ya afya.

Wananchi chukuweni tahadhari safari zenu

Serikali imewarai wananchi kujitafakari mara mbili kama kuna ulazima kwa kufunga safari kwenda katika maeneo ya Uganda ambayo yameripoti kuibuka maambukizi ya ugoinjwa huo.

Liberia | Roberts International Airport in Monrovia
Abiria wakiwasili baada ya safariPicha: Zoom Dosso/AFP/Getty Images

Kulikuwa na ripoti pia, serikali za mikoa hasa katika maeneo ya mkoa wa Kagera unaopakana na Uganda kwa kilometa 230 ulikuwa katika tahadhari kubwa huku maafisa wa afya wakiwa kwenye maeneo hayo kuimarisha usalama wa afya.

Mkurugenzi wa huduma za kinga Dr Beatrice Mutayoba amesema serikali inaendelea kutoa uzito kuhusu tahadhari ya kinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Soma Pia:Kenya yatangaza tahadhari ya Ebola Busia

Aidha amesema kuna haja ya wananchi kujielimisha kupitia wataalamu wa masuala ya afya juu ya virusi hivyo ambayo vinasababisha homa.

Kutokana na mazingira ya kijiografia, mbali ya mkoa wa Kagera unaotajwa kuwa hatarini zaidi kukumbwa na maambukizi ya ugonjwa huo,  pia kuna mikoa mingine kadhaa ambayo inatumbukia kwenye hatari ya aina hiyo.

Mikoa kama  Mwanza, Kigoma, Geita na Mara inaorodheshwa kwenye janga hilo na wananchi walioko kwenye maeneo hayo wameaswa kuchukua tahadhari zaidi.

Ugonjwa wa Ebola tayari umeyashambulia mataifa kadhaa barani Afrika ikiwemo Ugandaambayo imetangaza hivi karibuni, Jamhuri ya kidemocrasia ya Kongo na hata mataifa mengine ya Magharibi mwa Afrika.

Tanzania yajiandaa kukabilia na Ebola