Tamaduni za Pasaka zinazopendwa zaidi nchini Ujerumani
Chemchemi za Pasaka, moto wa kipagani, magurudumu ya moto na sungura waliofichwa: Kutoka Bavaria hadi Hamburg, hapa kuna mila 10 maarufu za Pasaka kote Ujerumani. Jiunge nasi kwenye safari ya sikukuu ya Pasaka
Yai la pasaka lililopambwa
Wajerumani wanapenda kuchora mayai ya Pasaka. Jamii ya walio wachache ya Wasorb huko Lusatia, Brandenburg, ni maarufu kwa sanaa yao ya kupamba mayai kwa nta. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu jamii ya walio wachace ya Slavic na desturi zao kwenye makavazi ya Spreewald huko Lübbenau.
Mti wa mayai ya pasaka
Kwa kawaida, Wajerumani hupamba miti au mashada ya maua kwa mayai ya rangi ya Pasaka. Mti wa mayai ya Pasaka wa Saalfeld unauweka utamaduni huu katika kiwango kipya. Mti huu umepambwa kwa mayai 10,000 ya Pasaka yaliopakwa rangi. Familia moja kutoka Saalfeld huko Thuringia ilianzisha utamaduni huu na sasa jiji hilo linauendeleza. Kila mwaka mti huu huvutia wageni wengi.
Maandamano ya pasaka
Hii ni desturi ya Wasorbia katika maeneo ya kikatoliki ya Lusatia. Wanaume hupita katika jamii za Wasorbia wakiendesha farasi waliopambwa ili kueneza habari za ufufuo wa Yesu Kristo. Kila mwaka, waendesha farasi hupitia katika eneo la juu la Lusatia huku watu wakitazama.
Matembezi ya wikendi ya Pasaka
Kwa Wajerumani wengi, kutembea ni lazima siku ya Pasaka. Utamaduni huu angalau unachochewa na shairi la "Matembezi ya Pasaka" la Johann Wolfgang von Goethe.
Kutafutwa kwa yai la pasaka
Kutafutwa kwa peremende na mayai yaliyofichwa na sungura wa Pasaka ni sehemu bora zaidi ya sikukuu hiyo kwa Wajerumani wengi wadogo. Huko Weimar, mji huo hupanga utafutaji rasmi kwa watoto kila mwaka
Sungura wa Pasaka
Desturi ya kwenda nje wakati wa Pasaka kutafuta mayai na zawadi ndogo zinazodaiwa kufichwa na sungura wa Pasaka imekuwa ikifanyika Ujerumani tangu karne ya 17. Wakati mwingine peremende na chakleti hufichwa kwenye vinyago vidogo vya umbo la sungura.
Moto wa Pasaka
Ni utamaduni ambao karibu kila mahali nchini Ujerumani huwashwa moto wa Pasaka. Desturi ya kipagani, ambayo inaadhimisha kuwasili kwa majira ya machipuko. Ulipitishwa na wakristo kuwakilisha ufufuo wa Kristo. Mioto minne mikubwa ya Pasaka huwashwa kwenye kingo za mto Elbe huko Hamburg. Miaka miwili iliyopita ilifutiliwa mbali kwasababu ya janga. Mwaka huu iliruhusiwa ingawa kwa kiwango kidogo.
Kuteketezwa kwa gurudmu la pasaka
Awali, ilikuwa desturi ya kipagani kusukuma magurudumu ya mbao yanayowaka moto chini ya kilima kukaribisha majira ya machipuko, tofauti na kuwashwa kwa moto. Hii leo, mila hiyo inaendelezwa Jumapili ya Pasaka huko Lüdge, North Rhine-Westphalia. Magurudumu haya ya Pasaka hutengenezwa kwa mwaloni na kujazwa na majani.
Msafara wa Ijumaa kuu huko Bensheim
Kila mwaka, maelfu hukusanyika katika mji wa Kusini-Magharibi wa Bensheim kutazama msafara unaoigiza kusulubishwa kwa Yesu Kristo. Utamaduni huu ulianzishwa na wafanyikazi wahamiaji waliokuja Ujerumani kutoka kusini mwa Italia. Ni utamaduni ambao pia hufanywa nchini Italia
Chemchemi za Pasaka za Franconia
Utamaduni wa kupamba chemchemi na visima kwa mayai ya Pasaka ilianza mapema karne ya 20 huko Franconia, Bavaria. Inaaminika kuwa eneo la milima la picturesque lilitaka kuvutia watalii na mila mpya ya kusherehekea maji, ambayo ni muhimu kwa maisha, na Pasaka, ambayo ni sherehe ya maisha mapya. Biberbach inajivunia mojawapo ya chemchemi kubwa zaidi za Pasaka nchini Ujerumani.