1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TALLINN : Ulaya na NATO waingilia mzozo wa Estonia

4 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC50

Umoja wa Ulaya na Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO wameingilia kati mzozo wa kidiplomasia kati ya Estonia na Urusi kutokana na kuondolewa kwa kumkumbu ya vita ya Urusi katika mji wa Tallinn nchini Estonia.

Umoja wa Ulaya na NATO wametaka mzozo huo utatuliwe kwa njia za kidiplomasia na wameitaka serikali ya Urusi kuwadhibiti vijana waliouzingira ubalozi wa Estonia mjini Moscow.Vijana hao wamesema kundi lao litaondoka kwenye ubalozi huo.

Wiki iliopita mamia ya Warusi walio wachache nchini Estonia walifanya ghasia mjini Tallinn kufuatia uamuzi wa serikali ya nchi hiyo kuhamisha kumbukumbu hiyo ya vita ya Urusi kutoka katikati ya jiji na kuipeleka makaburini.

Sanamu hiyo ya kumbukumbu ni kwa ajili kuadhimisha ushindi wa wanajeshi wa Urusi ambapo hapo mwaka 1945 waliwashinda wanajeshi wa Ujerumani.

Wananchi wa Estonia wanaliona sanamu hilo kama ishara ya utawala wa Urusi baada ya kipindi cha vita vikuu vya pili vya dunia.