1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Taliban yaombwa kubatilisha zuio la wanawake kufanya kazi

29 Desemba 2022

Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa kundi la mataifa saba tajiri duniani - G7 wametoa wito kwa serikali ya Taliban kubatilisha maramoja marufuku dhidi ya wanawake wanaofanya kazi nchini Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4LXV2
G7 Gipfel Elmau
Picha: Christinan Bruna/Getty Images

Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa kundi la mataifa saba tajiri duniani - G7 wametoa wito kwa serikali ya Taliban kubatilisha maramoja marufuku dhidi ya wanawake wanaofanya kazi katika sekta ya usambazaji misaada nchini Afghanistan. Marufuku hiyo ndiyo pigo la hivi punde dhidi ya haki za wanawake nchini Afghanistan tangu Taliban ilipochukua tena madaraka mwaka jana. Mawaziri hao wa G7 wamesema katika taarifa ya pamoja kuwa wana wasiwasi mkubwa kuwa amri hiyo isiyo ya haki na iliyo hatari inawaweka hatarini mamilioni ya Waafghanistan wanaotegemea msaada wa kiutu kwa ajili ya kuishi. Imejiri baada ya mashirika sita ya misaada kusitisha operesheni nchini Afghanistan kufuatia marufuku hiyo. Serikali hiyo ya msimamo mkali wa kiislamu pia mapema mwezi huu iliwazuia wanawake kusoma katika vyuo vikuu, hatua iliyozusha ukosoaji wa kimataifa na maandamano katika baadhi ya miji ya Afghanistan.