1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Taliban yaiomba dunia kuisaidia

17 Novemba 2024

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia Masuala ya Kisiasa nchini Afghanistan, Shir Mohammad Abbas Stanekzai, ameihimiza jumuiya ya kimataifa kuisaidia nchi yake.

https://p.dw.com/p/4n5gm
Afghanistan I Taliban
Wapiganaji wa kundi la Taliban nchini Afghanistan.Picha: Siddiqullah Alizai/AP/picture alliance

Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa mjini Kabul, Stanekzai ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali kutoa msaada kwa Afghanistan kwa njia ya misaada ya kiufundi, mipango ya maendeleo ya kiuchumi na ushirikiano wa kilimo.

Naibu Waziri huyo wa Mambo ya Nje amezikumbusha nchi ambazo hapo awali zilikuwa na wanajeshi nchini Afghanistan kwamba zina wajibu wa kimaadili katika kusaidia kuijenga nchi hiyo kwa kuzingatia Mkataba wa Doha.

Soma zaidi: Raia wa Afghanistan akamatwa kwa kula njama ya kufanya shambulio siku ya uchaguzi Marekani

Marekani na kundi la Taliban walitia saini makubaliano ya amani huko Doha ambayo yalihitimisha ukaliaji kimabavu wa Marekani nchini Afghanistan na hatimaye kurudi tena madarakani kwa watawala wa Taliban mnamo Agosti 2021.

Tangu wakati huo, serikali ya Taliban imekuwa ikitafuta kutambuliwa kimataifa na kupewa misaada, huku ukikabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kwa madai ya kuminya haki za wanawake.