1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaendelea na mazoezi ya kijeshi karibu na Taiwan

10 Aprili 2023

China imetoa onyo leo hii kwamba amani katika Ujia wa Bahari wa Taiwan na uhuru wa kisiwa hicho vina nafasi ya kipekee, wakati ikiendelea na mazoezi yake ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4Ps6D
Chinas dreitägige Militärübungen rund um Taiwan
Picha: Joint Staff Office of the Defense Ministry of Japan/REUTERS

Katika utaratibu wake wa kawaida wa taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Wang Wenbin, amesema kama kuna nia ya kulinda amani na utulivu katika Ujia wa Bahari wa Taiwan kwa nguvu zote lazima wapinge aina yoyote ya kujitenga kwa Taiwan.

Kwa upande, mwingine wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema imebaini meli 11 za kivita za China na ndege 59 katika maeneo yanayokizunguka kisiwa hicho.

Taarifa ya wizara hiyo imeongeza kwa kuthibitisha kuwa jeshi la China kwa upande wa mashariki linaendelea na mazoezi yake ya kijeshi karibu na Taiwan.