Tahadhari yatolewa dhidi ya MONUSCO kuondoka haraka Kongo
29 Septemba 2023Matangazo
Wiki iliyopita, Rais wa Kongo Felix Tshisekedi alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuharakisha zoezi la kuuondoa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, MONUSCO ambao umekuwa nchini humo kwa takribani miaka 25.
Tshisekedi amehimiza zoezi hilo lianze mwishoni mwa mwaka huu, badala ya Desemba 2024 kama ilivyopangwa.
Mwezi Desemba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kurefusha muda wa MONUSCO kuhudumu nchini Kongo, ingawa nchi hiyo imetilia shaka uwezo na ufanisi wa kikosi hicho kuwalinda raia katika kipindi cha miongo kadhaa ya ghasia za makundi ya wanamgambo wenye silaha.