1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa matano ya Sahel yafanya luteka

27 Mei 2024

Mataifa matano yaliyoko katika eneo la Sahel yamekuwa yakifanya luteka za kijeshi magharibi mwa Niger.

https://p.dw.com/p/4gKMD
Mapambano dhidi ya wanajihadi
Makundi ya kigaidi yameendelea kupanua ushawishi wao katika eneo la Sahel. Mashambulizi ya wanajihadi hutokea kila siku, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya kigaidi, mauaji na uvamizi kwenye vijiji.Picha: Inside the Resistance

Haya yamesemwa na wizara ya ulinzi ya Niger. Mazoezi haya ya kijeshi yanayofanywa na Burkina Faso, Chad, Mali, Niger na Togo ndiyo ya kwanza ya aina hiyo kufanyika katika eneo hilo lililozongwa na mashambulizi ya kijihadi.

Luteka hizo zinatarajiwa kufanyika hadi Juni 3. Tawala za kijeshi katika mataifa ya Burkina Faso, Niger na Mali, wamevifukuza vikosi vya Ufaransa kutoka kwenye mataifa yao na kwa sasa wanaonekana kuigeukia Urusi kwa uungwaji mkono.

Nchi hizo zilianzisha muungano wao wa ulinzi waliouita Muungano wa Mataifa ya Sahel na mwezi Februari walitangaza kujiondoa kutoka kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS.