Rais wa Marekani Joe Biden atilia mkazo sheria za kuvaa barakoa na kuagiza kuwekwa chini ya karantini kwa watu wanaosafiri kuelekea nchini humo, viongozi wa Umoja wa Ulaya wawataka raia wa bara hilo kutosafiri kiholela na kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Umoja wa Ulaya, wasisitiza wito wa kuachiwa huru kwa kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny