Tuliyo nayo asubuhi hii: Mamlaka mjini Berlin zinaendelea na jitihada za kumsaka mshukiwa wa shambulio la siku ya Jumatatu. Mawaziri wa Ujerumani wamepitisha muswada wenye lengo la kuongeza upelelezi katika jamii wakati hofu ya ugaidi ikizidi kuongezeka. Na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuunda jopo litakalo kusanya ushahidi kuhusu uhalifu wa kivita nchini Syria.