Matangazo
Mtu anayetarajiwa kuwa rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amerejea nyumbani kutoka uhamishoni, na kusema nchi yake imefungua ukurasa mpya wa demokrasia kamili. Kamanda wa jeshi la Waserb wa Bosnia Ratco Mladic amehukumiwa kifungo cha maisha kwa hatia ya mauaji ya halaiki na uhalifu mwingine wa kivita. Chama cha Social Democrats, SPD cha hapa Ujerumani, kinashinikizwa kufanya mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto na vyama vya kihafidhina chini ya uongozi wa Kansela Angela Merkel.