2 Aprili 2018
Matangazo
Rais Erdogan wa Uturuki na Waziri Mkuu Netanyahu wa Israel wameendelea kushambuliana vikali kwa maneno, kutokana na mauaji ya Gaza. Chama cha Kansela Merkel wa Ujerumani kimeingia kwenye kashfa ya kununua data za wapigakura katika uchaguzi wa mwaka jana. Na wanamgambo wa Al-Shabaab waripotiwa kuuwa wanajeshi wanne wa Uganda katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.