Chama tawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF chajiandaa kuanzisha mchakato wa kumtimua madarakani Rais Robert Mugabe, aliyekaidi miito ya kujiuzulu. Baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani, Kansela Angela Merkel asema anapendelea uchaguzi mpya kuliko serikali ya wachache. Rais Donald Trump aiweka Korea Kaskazini kwenye orodha ya nchi zinazoufadhili ugaidi.