Pande mbili pinzani nchini Libya na mataifa ya kigeni yanazoziunga mkono, kushiriki katika mkutano utakaoandaliwa mjini Berlin leo, wanajeshi 40 wa serikali ya Yemen wauawa katika shambulizi la kombora dhidi ya kambi ya kijeshi katika eneo la Mashariki la nchi hiyo na takriban watu 200 ikiwa ni pamoja na waandamanaji na polisi wajeruhiwa huku maandamano mapya yakigeuka kuwa ghasia mjini Beirut.