1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yainyoshea kidole Israel kwa mauaji ya Generali nchini Lebanon

Siraj Kalyango12 Desemba 2007

Umoja wa Ulaya umelaani mauji hayo

https://p.dw.com/p/Cam9

Syria imelaani mauaji ya afisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Lebanon katika mlipuko wa bomu uliotokea leo mashariki mwa mji wa Beirut.Ingawa wengi wanahisi kuwa imehusika kwa njia maoja au nyingine Syria kwa upande wake inaiyoshea kidole Israel.

Mlipuko wa bomu uliotokea mbele ya jengo la serikali mjini Lebanon, umewauwa watu wasiopungua wanne, akiwemo mwanajeshi mwandamizi ,Brigadier Generali Francois al-Hajj. Jengo hilo la serikali linaikaribia Ikulu ya rais ilioko katika mtaa wa Baabda wa wakristo wengi katika mji wa Beirut.

Shirika la habari la serikali ya Syria-SANA- linaihusisha Israel.Katika taarifa kulihusu shambulio la bomu la leo, limesema kuwa serikali ya Damascus inalilaani, na kuuendelea kuwa, linawalenga wanajeshi ambao wanapinga mwelekeo wa KiIsrael.Pia limeendelea kudai kuwa Israel na washirika wake nchini Lebanon ndio watafaidika na makosa ya kuuliwa kwa kiongozi mashuhuri kama huyo.Taarifa inamuelezae mwanajeshi huyo kama , alieunga mkono harati za kupinga Israel na aliekuwa anajaribu kuiunganisha Lebanon.

Shirika la habari la SANA linaendelea kudai kuwa Israel iliwahi kulilipua gari la mwanajeshi huyo mwaka 1976 baada ya kukataa kushirikiana na wanamgambo waliokuwa wakiunga mkono Israel katika eneo la kusini mwa Lebanon.Aidha linasema pia kuwa Israel ilimtishia al-Hajj wakati wa vita vya Lebanon mwaka wa 2006.

Duru ya kijeshi zinasema kuwa al-Hajj alikuwa mmoja wa watakaogombea nafasi ya kuchukua pahala pa mkuu wa majeshi, Generali Michel Suleman, ambae amechaguliwa na pande zote za bunge la Lebanon ,kuwa kiongozi ajayo wa Lebanon. Al Hajj, mbali na mengine,aliongoza operesheni za kijeshi dhidi ya kundi la wakereketwa la Fatah al- islam.Operesheni zilidumu miezi mitatu.

Nao umoja wa Ulaya, umehakikisha kuwa hauta –te-te-reka, katika juhudi zake za kuunga mkono hatua za Lebanon kuelekea demokrasia na kujiamulia mambo yake yenyewe bila kujali , mauaji ya Jenerali huyo.Taarifa iliotolewa na mkuu wa sera ya kigeni za umoja wa ulaya –Javier Solana, imesema kuwa umoja wa ulaya utaendelea na msimamo wake wa awali.

Syria imejihusisha sana katika masuala ya Lebabon tangu mwaka wa 1976 ilipotuma vikosi vyake huko wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipokuwa vikipamba moto mwezi Juni wa mwaka huo. Majeshi ya Syria yalikuwa yanaitikia mwaliko wa rais wa wakati huo, Suleman Franjieh, ambae nae ni wa dhehebu la kikatoliki la Maronite. Hata hivyo mauaji wa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon- Rafika Hariri mwaka wa 2005 ,yalipelekea majeshi ya Syria kuondoka huko na hivyo kukamilisha kipindi cha miaka 30 ya kuweko huko. Lakini Syria baado inawashirika huko, hususan kusini mwa Lebanon, sana sana- kundi la Kishia la Hezbollah, ambalo linafikirwa kudhaminiwa na Iran.