1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Syria yafanya uchaguzi wanne wa Bunge tangu kuzuka kwa vita

15 Julai 2024

Wasyria katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali wanapiga kura leo katika zoezi la uchaguzi wa nne wa bunge tangu nchi hiyo ilipotumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011.

https://p.dw.com/p/4iJas
Syria l Uchaguzi wa Bunge mjini Damascus
Uchaguzi wa Bunge nchini Syria.Picha: Ymam Al Shaar/REUTERS

Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kukipa ushindi chama tawala cha rais Bashar al Assad cha Baath na kukibakisha madarakani.

Zoezi la uchaguzi limeripotiwa kufanyika kwa utulivu katika maeneo mengi ingawa vyombo vya habari la mashirika ya kufuatilia vita yameripoti kutokea maandamano ya kupinga zoezi hilo la uchaguzi katika mkoa wa Sweida ulioko Kusini mwa Syria.

Mkoa huo unakaliwa na idadi kubwa ya jamii ya wachache ya  Wadruze. Zaidi ya watu 1500 wanagombea viti 250 vya bunge la nchi hiyo.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW