1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY:Cheney-litakuwa kosa kuiruhusu Iran kuwa na nguvu ya nyuklia

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCP3

Marekani haifutilii mbali uwezekano wa kuchukuliwa hatua ya kijeshi dhidi ya Iran ikiwa Teheran haitositisha mradi wake wa nyuklia.Naibu rais wa Marekani,Dick Cheney aliposhiriki katika mkutano wa waandishi wa habari pamoja na waziri mkuu wa Australia John Howard alisema litakuwa kosa kubwa kuiruhusu Iran kuwa dola lenye nguvu ya nyuklia.Wakati huo huo akasema kuwa milango ipo wazi kutafuta njia zingine za kusuluhisha mgogoro huo.Serikali ya Teheran imepuuza ule muda uliowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,kwa nchi hiyo kusitisha mradi wake wa nyuklia.Sasa Iran inakabiliwa na kitisho cha kuwekewa vikwazo vipya.