1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SYDNEY: Mfungwa wa Guantanamo arejea nyumbani

20 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0L

Muaustralia David Hicks aliekuwa mfungwa katika jela ya Guantanamo Bay amerejea nyumbani kumaliza kifungo chake katika jela yenye ulinzi mkali, nchini Australia.Hicks,mwenye miaka 31 alikamatwa Afghanistan mwishoni mwa mwaka 2001 na alizuiliwa katika jela ya kijeshi ya Marekani ya Guantanamo Bay kwa muda wa miaka mitano.Mwezi Machi mwaka huu alipewa kifungo cha miaka saba na halmashauri ya kijeshi ya Marekani baada ya kukubali makosa ya kutoa msaada kwa Al-Qaeda nchini Afghanistan.Lakini kuambatana na maafikiano yaliyopatikana pamoja na waendesha mashtaka,sehemu kubwa ya kifungo hicho kilipunguzwa hadi miezi tisa.Sasa,Hicks atatumikia kifungo cha miezi saba iliyobaki katika jela ya Australia.Kurejeshwa kwake nyumbani kunahitimisha kampeni ya miaka mitano iliyokuwa ikifanywa na familia yake na baadhi kubwa ya umma.Waziri Mkuu wa Australia,John Howard ametuhumiwa vikali kuwa aliipuza kesi ya Hicks licha ya familia,marafiki na umma kufanya kampeni ya kutaka kumrejesha nyumbani Hicks,tangu miaka mitano iliyopita.