1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sweden yasema bado haijulikani aliyehujumu Nord Stream 2

7 Aprili 2023

Mamlaka ya mashtaka nchini Sweden imesema mpaka sasa bado haijulikani ni nani aliyehusika na uharibifu wa bomba la gesi la Nord Stream 2 katika Bahari ya Baltic.

https://p.dw.com/p/4PoSD
Lubmin | Nord Stream 2
Picha: Fabrizio Bensch/REUTERS

Mwendesha mashtaka ya umma nchini humo, ameongeza kuwa ufadhili wa serikali ndio hali kuu wanayochunguza. Mwendesha huyo wa mashtaka amesema bado anatumai kuthibitisha ni nani aliyetenda uhalifu huo lakini imekuwa vigumu kutokana na mazingira yaliopo. Bomba hilo la Nord Stream 2 linalosafirisha gesi kutoka Urusi kueleka Ujerumani, liliharibiwa katika mfululizo wa milipuko mnamo mwezi Septemba. Kulingana na mamlaka ya Sweden, mabaki ya vilipuzi yalipatikana kwenye bomba hilo lililoharibika. Mamlaka ya Ujerumani pia imekuwa ikichunguza tukio hilo, huku waendesha mashtaka mwezi uliopita wakitangaza kuwa meli inayoshukiwa kuhusika na milipuko ya bomba hilo ilimefanyiwa uchunguzi.