JamiiUswidi
Sweden yamtia hatiani mtuhumiwa wa kwanza wa kuchoma Quran
12 Oktoba 2023Matangazo
Hii ni mara ya kwanza kwa mfumo wa mahakama nchini humo kumshitaki mtu kwa kunajisi kitabu kitakatifu cha Uislamu.
Hukumu hiyo imetolewa baada ya wimbi la uchomaji moto Quran mapema mwaka huu hali iliyozusha ghadhabu kote ulimwenguni na kuifanya Sweden kulengwa, hatua iliyosababisha shirika la kijasusi la nchi hiyo kuongeza tahadhari dhidi ya ugaidi.
Serikali ya Sweden ililaani visa hivyo vya kuchoma moto Quran, ingawa iliendelea kusisitizia juu ya sheria zinazotoa uhuru mpana wa kujieleza.
Mahakama ya wilaya ya Linkoping ilimtia hatiano kijana huyo wa miaka 27 kwa kosa la uchochezi wa kikabila, ikisema hatua yake imewalenga Waislamu na sio Uislamu kama dini.