Makala ya Sura ya Ujerumani leo hii inauangazia mtandao wa Colmena na jinsi unavyowasaidia waandishi wa habari. Mtandao huo unawawezesha kukusanya habari na kuziwasilisha kupitia mtandao kutokea mahali popote. Wawakilishi wa vyombo vya habari mbalimbali kutoka nchi zilizopo Amerika ya Kusini na bara la Afrika walishiriki katika uzinduzi huo wa mtandao wa Colmena uliofanyika Berlin Aprili, 28.