1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Super Mario akaribishwa tena Uingereza

22 Agosti 2014

Soka la Uingereza linamkaribisha tena mmoja wa wachezaji wenye utata kabisa. Liverpool ilimuuza mchezaji Luis Suarez na sasa wamemnunua Mario Balotelli ili kulijaza pengo la mashambulizi

https://p.dw.com/p/1CzSS
WM 2014 Gruppe D 1. Spieltag England Italien
Picha: Reuters

Klabu ya AC Milan ya Italia imemruhusu Balotelli mwenye umri wa miaka 24 kuhamia Anfield katika uhamisho unaokisiwa kugharimu pauni milioni 16 kwa mujibu wa ripoti nchini Italia na Uingereza. Liverpool itamhitaji Baloteli kubadilisha tabia zake na kuzingatia nidhamu ya hali ya juu wakati akiichezea klabu hiyo.

Balotelli yuko nchini Uingereza kwa ajili ya vipimo vya matibabu kabla ya kukamilisha uhamisho wake kabla ya kujiunga na wenzake katika uwanja wa Anfield

Balotelli anatarajiwa kuchukua nafasi iliyowachwa na mchezaji mwingine aliyekumbwa na utata Luis Suarez ambaye alihamia Barcelona. Hhmm tutasubiri tu kuona kama kweli Super Mario atausikiwa wito wa kumtaka aache sakata na vituko vyake baada ya kurudi tena Uingereza.

Mwandishi: Bruce AMANI/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu