Sumu yadaiwa kuuwa Syria
21 Agosti 2013Madai hayo yanatolewa wakati timu ya watu 20 ya Umoja wa Mataifa ikiwa nchini Syria kwa ajali ya kuchunguza madai ya kutumiwa silaha za kemikali katika miji mitatu tofauti nchini humo ambayo inadaiwa kutumika silaha hizo za maangamizi.
Hata hivyo serikali ya Syria imeibuka na kukanisha vikali madai hayo ya kutumia silaha za kemikali katika shambulizi hili la sasa. Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa hilo SANA, likinukuu chanzo ambacho hakukutaka kutaja jina lake kikisema "Taarifa hiyo ni jaribio la kupoteza malengo ya timu ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kutekeleza vyema wajibu wake".
Uzito wa mashambulizi
Shirika la uangalizi wa haki za binaadamu la Syria lenye makao yake mjini London, limesema mashambulizi yalikuwa makali sana na yalilenga viunga vya Damascus kwa upande wa mashariki, maeneo ya Zamalika, Arebeen na Ein Tarma.
Katika taarifa yake shirika hilo limemnukuu, mwanaharakati akisema majeshi ya serikali yamefyatua mareketi yenye hewa ya sumu, na kuuwa watu kumi. Rami Abdul-Rahman, mkuu wa shirika hilo alitilia mkazo kauli hiyo kwa kusema wamepata taarifa za kufyatuliwa hewa ya yenye sumu kwa kumia maroketi sambamba na maeneo mengine ya angani.
Kundi lingine la wanaharakati limesema mamia ya watu wameuwawa au kujeruhiwa kufatia kutokana na mashambulizi hayo. Kuwepo kwa takwimu tofauti za vifo au majeruhi kutoka nchini Syria imekuwa kawaida unapotokea mkasa kama huo kwa kuwa kuzuia waandisha wa nje wa ndani kuripoti kuhusu mambo yanayojitokeza.
Zaidi ya watu 40 wameuwawa
Abdul-Rahman amesema zaidi ya watu 40 wamethibitishwa kuuwawa na kwamba vifo hivyo vitegemewe kuongeza mpaka kufikia watu 200 katika vitongoji vya jiji la Damascus.
Serikali imekanusha madai ya upande wa upinzani kwamba inatumia silaha za kemikali, kwa kusema waasi wanaopigana kumuondoa Bashar al Assad wamewahi kutumia silaha hizo.
Kufuatia repoti za leo hii, wanaharakati wametoa wito kwa timu ya Umoja wa Mataifa iliyopo nchini Syria kwa sasa na asasi nyingine za kimataifa kufika katika maeneo yalikufanyika mashambulizi kwa lengo la kufanikisha haraka upatikanaji wa matibabu na misaada mingine ya kiutu pamoja na kufanya uchunguzi wa kina kuhusu shambulizi hilo.
Mwanaharakati mwingine katika eneo hilo Mohammed Said amesema idadi kubwa watu walikufa na majeruhi imewahishwa katika hospitali moja iliyopo mashariki mwa viunga vya Damascus.
Madai haya ya leo ya kutimika kwa silaha za kemikali kama yatathibitishwa litakuwa tukio kubwa zaidi kufanyika zaidi ya lile la Machi 19 katika eneo la Khan al-Assal ambalo zaidi ya watu 30 walipoteza maisha na upande wa Assad na waasi wanalaumiana kufuatia shambulio hilo.
Mwandishi: Sudi Mnette APE
Mhriri:Yusuf Saumu