SiasaSudan
Sudan yatishiwa na maandamano mapya
31 Januari 2023Matangazo
Vikosi vya usalama vimeendesha ukandamizaji dhidi ya maandamano kama hayo tangu jeshi lilipotwaa madaraka, na kuuwa watu wasiopungua 100, kwa mujibu wa chama cha madaktari kinachoegemea makundi ya kudai demokrasia. Katika mji mkuu Khartoum, waandamanaji watajaribu kuandamana kuelekea kasri ya rais ambako wana uhakika wa kukumbana na askari polisi waliojihami pakubwa. Na kama ilivyoshuhudiwa katika maandamano mengine, mamlaka huenda zikayafunga madaraja mjini Khartoum ili kuzuwia waandamanaji kukusanyika. Maandamano ya kudai demokrasia yameendelea nchini Sudan licha ya makubaliano ya Desemba kati ya jeshi la makundi ya upinzani ya kiraia kukomesha mzozo wa kisiasa wa taifa hilo.