1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan yapinga kuushambulia ubalozi wa UAE

30 Septemba 2024

Jeshi la Sudan leo limepinga lawama zilizotolewa na Umoja wa Falme za Kiarabu kwamba vikosi vya jeshi hilo la Sudan vilishambulia kwa mabomu makazi ya balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu mjini Khartoum.

https://p.dw.com/p/4lEVi
Sudan | Abdel Fattah al-Burhan
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan, Abdel Fattah al-Burhan.Picha: AFP

Jeshi la serikali badala yake limeelekeza lawama hizo kwa wanamgambo wa RSF.

Katika taarifa yake limesema matendo haya ya aibu na ya woga yanafanywa na vikosi vya RSF vinavyoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo.

Soma zaidi: Mashambulizi ya siku mbili ya RSF huko El-Fasher yaua watu 48

Jeshi la Sudan mara kwa mara limekuwa likiushutumu Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kutoa silaha na msaada kwa vikosi vya RSF katika vita vilivyodumu kwa miezi 17.

Taifa hilo la Ghuba limekanusha madai hayo.