Uhusiano kati ya Sudan na Ethiopia umedhoofika katika miaka ya hivi karibuni juu ya eneo la ardhi yenye rotuba la mpakani la Fashaqa. Eneo hilo linagombaniwa na nchi zote mbili. Saidi Msonga ni mchambuzi wa masuala ya Diplomasia na siasa za kimataifa, tulimuuliza mzozo huu una athari gani kwa mataifa haya mawili na bara Afrika kwa ujumla?