Strassbourg. Ufaransa. Gul atetea rekodi ya Uturuki ya haki za binadamu.
4 Oktoba 2007Rais wa Uturuki Abdullah Gul ametetea rekodi ya nchi yake ya haki za binadamu katika kikao muhimu cha umoja wa Ulaya, lakini amekiri kuwa iko haja ya kujishughulisha zaidi. Umoja wa Ulaya umeitaka Uturuki kuondoa kifungu namba 301 katika sheria ya nchi hiyo, ambayo inafanya kuwa ni uhalifu kuutusi utaifa wa Uturuki ama taasisi za nchi.
Gul amewaambia wabunge wa bunge la Ulaya katika mji wa Strassbourg nchini Ufaransa kuwa anataka kuona kuwa kifungu hicho kinafanyiwa mabadiliko , na kudokeza kuwa kimechafua taswira ya Uturuki , wakati inajaribu kufanya majadiliano ya kupata uanachama wa umoja wa Ulaya.
Amesema kuwa aina zote za ubaguzi zimepigwa marufuku. Uhakikisho wa kisheria na kikatiba kuhusiana na haki ya mikusanyiko na uanachama unatekelezwa. Haki za kitamaduni na dini zinaongezwa. Ni vigumu kupambana na nchi mwanachama wa baraza la Ulaya inayotumia njia za kisasa zaidi za utesaji kuliko Uturuki, amesema Gul.
Waendesha mashtaka wazalendo nchini Uturuki wametumia kifungu hicho 301 dhidi ya waandishi, wanahabari na wasomi kadha, ikiwa ni pamoja na mshindi wa nishani ya fasihi Orhan Pamuk licha ya kuwa kesi hizo hazifikii mtu kuhukumiwa kwenda jela.