1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stockholm:Mkutano dhidi ya ukeketaji

11 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEEa

Mkutano wa kimataifa wa siku mbili
wa kuzuia zoezi la Wanawake
kukeketwa barani Afrika na miongoni
mwa familia za Wahamiaji nchini
Sweden unaofanywa Stockholm
unatarajiwa kumalizika leo.
Wanaoshiriki mkutanoni wametoa mwito
wa kushirikiana zaidi kwa lengo la
kukomesha mila hizo. Maafisa wa
serikali ya Sweden wamesema kuwa
Wasichana na Wanawake wapatao
millioni 130 ulimwenguni kote
wamekeketwa wakati ambapo wengine
millioni mbili hukeketwa kila mwaka.
Maafisa hao wameongeza kusema kuwa
jinsi Wahamiaji wa Kiafrika
wanavyozidi kuwa wengi nchini Sweden
ndivyo ambavyo tatizo hili limekuwa
la kitaifa katika nchi za
Scandinavia. Miongoni mwa wale
wanaohudhuria mkutano huo ni Wajumbe
kutoka nchi kumi za Kiafrika ambazo
ukeketaji ni jambo la kawaida.
Baadhi ya nchi hizo ni Tanzania,
Kenya, Somalia, Eritrea, Ethiopia,
Mali, Nigeria, Senegal na Misri.
Mkutano wa Stockholm unahudhuriwa
pia na Wajumbe wa Umoja wa Mataifa,
Wabunge na mashirika ya kiutu.