Stockholm.Misaada yatolewa kuijenga upya Lebanon.
31 Agosti 2006Ujerumani imeahidi msaada wa Euro milioni 22 katika ujenzi mpya wa nchi ya Lebanon iliyoharibiwa kwa mashambulizi ya Israel.
Waziri wa maendeleo wa Ujerumani Heidemarie Vitsoghek-Tsoel ametangaza hilo katika mkutano wa wachangiaji wa kimataifa katika mkutano uliofanyika Stockholm.
Akitoa taarifa kwa wawakilishi katika mkutano huo waziri mkuu wa Lebanon Fuad Siniora amewataka wachangiaji hao kufanya kila liwezekanalo kuisaidia nchi hiyo katika kuijenga upya kufuatia kuharibiwa kutokana na vita kati ya Israel na Hezbollah.
Katika hotuba yake katika kulaani mashambulio hayo yaliyofanya na Israel katika nchi yake Siniora amesema.
“Uvamizi huu wa sasa katika miundo mbinu na milki binafsi za watu, umesababisha hasara katika pato la ndani, hasara katika nafasi za kazi na hasara za moja kwa moja na zisizo za moja kwa mojaza kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kupotelewa na hasara ya mapato katika sekta ya Utalii, kilimo na viwanda. Zaidi ya hayo ufanisi uliopatikana Lebanon katika miaka 15 baada ya vita umezolewa kufumba na kufumbua na vyombo vya kivita vya Israel”.