1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STOCKHOLM: Wafadhili wameahidi kuisaidia Lebanon

1 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDGH

Katika mkutano wa kimataifa mjini Stockholm, madola fadhili yameahidi kutoa zaidi ya Euro milioni 730,kusaidia ujenzi upya nchini Lebanon. Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa Sweden,Jan Eliasson,msaada ulioahidiwa na wafadhili ni mkubwa zaidi ya vile ilivyotarajiwa. Ujerumani,imeahidi kutoa msaada wa Euro milioni 22.Waziri mkuu wa Lebanon Fuad Siniora aliehudhuria mkutano huo nchini Sweden, ameyashukuru madola fadhili na amehakikisha kuwa pesa hizo hazitokwenda kwa Hezbollah.Akaziomba nchi fadhili kusaidia iwezekanavyo kuijenga upya Lebanon kufuatia vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah.Mkutano huo ulifungwa kwa kutoa mwito kwa Israel kondosha vikwazo vya anga,bahari na ardhi kavu vilivyowekwa dhidi ya Lebanon.