STOCKHOLM : Mamilioni kusaidia ujenzi wa Lebanon
1 Septemba 2006Hapo jana ikiwa ni siku ya kwanza ya mkutano wa wafadhili kuisaidia Lebanon nchi fadhili zimeahidi kutowa zaidi ya euro milioni 730 katiika msaada wa ujenzi mpya wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na euro milioni 22 kutoka Ujerumani.
Maafisa wanasema kima hicho kimepindukia mno matarajio yao.Kwa kuzingatia ahadi zilizotolewa huko nyuma takriban euro bilioni moja hivi sasa zinapatikana.
Waziri wa ushirikiano wa maendeleo wa Ujerumani Heidemarie Wieczorek Seul anasema.
Waziri Mkuu wa Lebanon Fuad Siniora ameishukuru jumuiya ya Kimataifa kwa msaada huo na kusema kwamba atahakikisha kwamba fedha hizo hazitoishia kwenye mikono ya wanachama wa siasa kali wa kundi la Hizbollah
Mkutano huo ulimalizika kwa taarifa kutoka nchi wafadhili zikitowa wito kwa Israel kuondosha vikwazo vyake vya anga baharini na ardhini kwa Lebanon.