Steinbrück mgombea wa SPD kiti cha kansela
2 Oktoba 2012Gazeti la Neue Osnabrücker Zeitung, likizungumzia kuhusu uteuzi wa Steinbrück kugombea kiti cha ukansela katika uchaguzi utakaofanyika mwakani, linaandika:
"Steinbrück jana alivuka kikwazo kingine katika njia yake kuelekea kuwa mgombea wa chama cha SPD. Kura za uongozi wa chama hicho zinajionyesha wazi. Hii ina maana , bawa la kushoto la chama hicho linaonekana kupata shauku zaidi na Steinbrück na limeendelea kumuunga mkono. Kwa upande wa bawa hilo la kushoto la SPD , pia lengo lao ni kurejea katika nguvu za uongozi wa serikali, ili kuweza kuelekeza tofauti wanazolenga za kisiasa".
Gazeti la Nürnberger Zeitung, likizungumzia kuhusu mada hiyo, linaandika:
"Steibrück , iwapo leo hii angekuwa farasi, ambaye hana uzoefu wa mashindano ya kimataifa, lakini amepewa uwezo wa kwenda mbio, Iwapo itawezekana kumsimamisha , hilo ni suala la kujadiliwa . Kwa upande wa ushindi hii bila shaka ni njia ambayo amekwisha pitia, kama utaangalia kwa upande wa wakati alipokuwa waziri wa fedha wa Ujerumani. Lakini wakati huo chama chake kilikuwa mshirika wa kansela wa sasa , ambapo maoni ya wapiga kura yanaonyesha kuwa bado chama chake kiko nyuma".
Mada nyingine iliyowashughulisha wahariri ni kuhusu mjadala unaoendelea katika baraza kuu la umoja wa mataifa kuhusu Syria. Mhariri wa gazeti la Märkische Oderzeitung la mjini Frankfurt anaandika:
"Umoja wa mataifa unaonyesha kwa mara nyingine tena , kuwa si chombo ambacho kinaweza kuleta suluhisho katika mizozo, kama ilivyokusudiwa, kutokana na picha ya dunia hii inavyojionyesha. Madaraka yake yamekwama, lakini hakuna ajuwae, iwapo itawezekana kuanzisha taasisi nyingine kama hii ambayo itafanyakazi vizuri zaidi. Ama iwapo hiyo itakuwa bora zaidi kuliko hii tuliyonayo".
Kuhusu mada hiyo, gazeti la Hannoversche Allgemeine Zeitung linaandika.
"Mwishoni mwa mwaka huu Ujerumani itaondoka katika baraza la usalama la umoja wa mataifa baada ya kuwapo huko kwa muda wa miaka miwili. Tathmini ya miaka hii miwili ni mbaya. Vuguvugu la mageuzi katika mataifa ya Kiarabu limekuja bila ya umoja wa mataifa kujua na kujitayarisha. Hivi leo Urusi na China zinazuwia kwa kutumia kura ya veto, uwezo wa kuwalinda raia wa Syria dhidi ya serikali yao. Haishangazi basi , kwamba wakosoaji wa umoja wa mataifa wameanza kujitokeza. Mkataba wa umoja wa mataifa unatajwa kuwa ni chombo kitakacholeta maafa makubwa kwa dunia kuhusiana na vita. Haki ya kuwa na kura ya veto inaonekana hii leo kuwa kinyume chake".
Kwa upande wa siku ya muungano wa Ujerumani, gazeti la Berliner Morgenpost linaandika:
"Helmut Kohl , ambaye katika siku hii , iwapo kuchaguliwa kwake kuwa kansela miaka 30 iliyopita kulithaminiwa , hii inaweza kuangaliwa katika kiwango kingine kisiasa, kwamba alileta muungano , na mshikamano katika bara la Ulaya , na pia katika uchumi ni kwamba , kumekuwa na umoja wa kiuchumi pia. Kisiasa , alikuwa na mtazamo wa kuwa na Ulaya ambayo ni nguzo ya amani. Kwasababu , kwa kutaka kuepuka hali ya kutoaminiana, Kohl aliona haja ya kuiunganisha nchi ya Ujerumani. Hata hivyo hatua za muungano wa Ujerumani na Ulaya bado zinaendelea ,kuwa katika hatua za mabadiliko".
Mwandishi : Sekione Kitojo / Inlandspresse
Mhariri: Mohammed Khelef