Spika wa Bunge la DRC Vitali Kamehre ajiuzulu
25 Machi 2009Matangazo
Kwa muda mrefu Spika huyo amekuwa katika mvutano mkubwa na Rais Joseph Kabila kutokana na hatua ya kiongozi huyo kuwaalika wanajeshi wa Rwanda kujiunga na jeshi la nchi hiyo kupambana na waasi wa Rwanda wa kundi la FDLR mashariki mwa Kongo.
Mwandishi wetu Salehe Mwanamilongo alioko Kinshasa amezungumza na mbunge wa chama tawala Ramadhani Shadari pamoja na mbunge wa upinzani wa chama cha MLC Francois Mwamba.