1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SPD kitaendelea kutawala Jimbo la Berlin

19 Septemba 2011

Siasa katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin zitaendelea kuwa na mhuri wa chama cha SPD, baada ya chama hicho kujinyakulia takriban asilimia 30 ya kura katika uchaguzi uliyofanywa hapo jana katika jimbo la Berlin.

https://p.dw.com/p/RmVE
Berlin's Regierender Buergermeister Klaus Wowereit waehrend eines Landesparteitages der SPD in Berlin am Samstag, 20. Mai 2006. Wowereit wurde erneut zum Spitzenkandidaten fuer die Senatswahlen im September gewaehlt. (AP Photo/ Jan Bauer) --- Berlin mayor Klaus Wowereit during a Social Democrats' party local convention in Berlin on Saturday, May 20, 2006. Wowereit was elected as the new top candidate for the September state elections in Berlin. (AP Photo/ Jan Bauer)
Meya wa Berlin, wa chama cha SPD, Klaus WowereitPicha: AP

SPD tena kimeibuka chama chenye nguvu kubwa kabisa katika bunge la jimbo la Berlin. Lakini Meya wa sasa Klaus Wowereit alieshinda kwa mara ya tatu mfululizo, atapaswa kutafuta mshirika mpya baada ya kushirikiana na Die Linke katika serikali ya mseto kwa miaka 10. Chama cha Kijani kilichojikingia takriban asilimia 18 ya kura, kinatazamiwa kuwa na nafasi nzuri ya kushirikiana na SPD kuunda serikali ya mseto. Hata CDU kilichopata kama asilimia 23 ya kura kinaweza kushirikiana na SPD katika serikali ya muungano mkubwa. FDP kimepata pigo kubwa baada ya kupata chini ya asilimia 2 na hivyo hakitokuwepo katika bunge la jimbo la Berlin.

Chama kilichowashangaza wengi, ni Die Piraten kilichoundwa na wanaharakati wa mtandao wa internet miaka mitano iliyopita. Kwa mara ya kwanza kabisa chama hicho, kimefanikiwa kuingia bungeni nchini Ujerumani baada ya kujinyakulia takriban asilimia 9 ya kura katika uchaguzi wa hapo jana.

Journalisten richten am Sonntag (18.09.11) in der Kulturbrauerei in Berlin bei der Wahlparty der SPD nach der Bekanntgabe der ersten Prognose zur Wahl des Abgeordnetenhauses ihre Kameras auf einen jubelnden Anhaenger. Am Sonntag waren 2,47 Millionen wahlberechtigte Berliner aufgerufen, das Abgeordnetenhaus und die Bezirksverordnetenversammlungen zu waehlen. (zu dapd-Text) Foto: Clemens Bilan/dapd
Wafuasi wa SPD wakisherehekea ushindiPicha: dapd

Wafuasi wa SPD tangu muda mrefu walikuwa na hakika ya kuibuka washindi. Baada ya matokeo ya uchaguzi kudhihirisha ushindi wao, Meya wa Berlin Klaus Wowereit alieshangiriwa na wafuasi wake alipoingia kwenye ukumbi walikokusanyika aliwaambia:

"Nahisi raha kuwa pamoja nanyi. Kwenye televisheni nimeziona sherehe za uchaguzi za vyama vingine. Nabidi kusema sherehe zetu ni nzuri na bora zaidi. Ahsanteni kwa msaada wenu."

Kuna uwezekano mkubwa kwa SPD kuunda serikali pamoja na chama cha Kijani, hasa kwa kuzingatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 kwa matumaini ya kuipiga kumbo serikali ya mseto ya wahafidhina na waliberali inayoongozwa na Kansela Angela Merkel. Lakini kwanza, SPD na chama cha Kijani, vitapaswa kudhihirisha uwezo wa kushirikiana katika serikali ya jimbo la Berlin.

Vyama hivyo viwili vikishindwa kuafikiana, basi Meya Wowereit anaweza kuunda serikali pamoja na CDU, lakini hata hapo kuna wasiwasi kwani chama hicho hakitoelewana na SPD na matarajio yake katika sera za serikali kuu.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa FDP alie pia waziri wa uchumi, Philip Rösler alitamka hadharani juu ya kuwepo uwezekano mkubwa kwa Ugiriki kufilisika. Matamshi hayo ni kinyume kabisa na msimamo wa Kansela Merkel. Kwa maoni ya mwenyekiti wa chama cha Kijani Claudia Roth, FDP kimeadhibiwa katika uchaguzi wa Berlin. Amesema:

" Nimefurahi sana kuwa FDP na sera zake dhidi ya Ulaya katika serikali kuu ya Berlin, kimeadhibiwa katika mji mkuu wetu. Natazamia kuwa Kansela Merkel sasa atachukua hatua za kweli."

Anhaenger der Piratenpartei feiern am Sonntag (18.09.11) in Berlin in dem Club Ritter Butzke auf der Wahlparty der Piratenpartei die ersten Hochrechnungen fuer die Wahl zum Berliner Abgeordnetenhaus. Am Sonntag waren 2,47 Millionen wahlberechtigte Berliner aufgerufen, das Abgeordnetenhaus und die Bezirksverordnetenversammlungen zu waehlen. (zu dapd-Text) Foto: Adam Berry/dapd
Die Piraten kimeingia bungeni mara ya kwanza kabisaPicha: dapd

Kwa upande mwingine, Die Piraten kilichoundwa miaka mitano iliyopita tu, kimeingia bungeni kwa mara ya kwanza kabisa. Watu wanauliza kipi kilichowafanya wapiga kura 120,000 kukichagua chama hicho. Suala jingine ni kwanini kama asilimia 40 ya wakaazi miloni mbili na nusu walio na haki ya kupiga kura, hawakwenda kuitumia haki hiyo.

Mwandishi: Fürstenau,Marcel/ZPR

Mhariri: Mwadzaya, Thelma