Somalia
4 Januari 2009Matangazo
Waandishi habari wawili wa kigeni,mmoja wa kiengereza na mwengine mpiga picha wa kutoka Hispania,waliotekwa nyara November 26 mwaka jana,katika eneo la kaskazini mwa Somalia, lililojitangazia utawala wa ndani-Puntland,wameachiwa huru hii leo.Habari hizo zimetangazwa na afisa wa ngazi ya juu wa polisi huko Puntland.