1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia

Oumilkher Hamidou30 Novemba 2008

Baraza la wenye busara laitaka jumuia ya kimataifa iwajibike haraka nchini Somalia

https://p.dw.com/p/G6CY

Nairobi:


Kundi la wenye busara la umoja wa Afrika limelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa litume kikosi cha kimataifa ,bila ya kupoteza wakati nchini Somalia.Mwito huo umefuatia uamuzi wa Erthiopia wa kuwarejesha nyumbani wanajeshi wake hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2008.Kundi la wenye busara-taasisi ya Umoja wa Afrika inayowaleta pamoja marais mashuhuri wa zamani wa kiafrika,limelihimiza baraza la Usalama liwajibike kikamilifu nchini Somalia.Katika taarifa yake iliyochapishwa mjini Nairobi, taasisi hiyo ya Umoja wa Afrika imesema inahofia vurumai na mtafaruku visije vikazidi kukorofisha juhudi za amani na suluhu ya kudumu.Wazee wenye busara wa umoja wa afrika wameitolea mwito pia jumuia ya kimataifa iwajibike zaidi katika kusaka ufumbuzi wa kudumu wa mzozo wa Somalia.