1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yasema watu 24 wafa baada ya boti mbili kupinduka

Josephat Charo
25 Novemba 2024

Shirika la Umoja linaloshughulikia uhamiaji IOM limewahi kuelezea wasiwasi wake kuhusu uhamiaji usio halali kutoka eneo la Pembe ya Afrika huku watu wakikimbia mizozo na ukame.

https://p.dw.com/p/4nNov
Eneo la pwani ya Madagascar
Eneo la pwani ya MadagascarPicha: AFP via Getty Images

Watu 24 wamekufa baada ya boti mbili kupinduka nje ya pwani ya Madagascar katika bahari ya Hindi. Hayo ni kwa mujibu wa serikali ya Somalia.

Waziri wa mambo ya nje wa Somalia Ahmed Moalim Fiqi amesema watu 46 wameokolewa. Fiqi amesema wanafanya kila wanaloliweza kuhakikisha walionusurika wanarejeshwa nyumbani salama na kupewa huduma inayohitajika.

Abiria wengi katika boti hizo walikuwa vijana raia wa Somalia na walikokuwa wakielekea hakujafahamika.

Ujumbe unaongozwa na balozi wa Somalia nchini Ethiopia umepangiwa kusafiri kwenda Madagascar kuchunguza tukio hilo na kuratibu juhudi za kuwasaidia walionusurika.