1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yapinga majeshi ya Kenya kwenye ardhi yake

25 Oktoba 2011

Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Ahmed, amesema kwamba haikubaliki kwa majeshi ya Kenya kuweko Somalia bila ya kutolewa kibali na serikali yake, msimamo ambao unachukuliwa kuwa ni tafauti sana na ilivyofahamika mwanzoni.

https://p.dw.com/p/12yJz
Mwanajeshi wa Kenya akipanda lori kuelekea Somalia.
Mwanajeshi wa Kenya akipanda lori kuelekea Somalia.Picha: dapd

Tamko hilo ambalo ni kali kabisa kutolewa hadi sasa na serikali ya Somalia kupinga kujiingiza majeshi ya Kenya katika nchi hiyo tangu wiki moja iliopita, linazua utata wa kimahusiano baina ya Kenya na Somalia. Jana majeshi ya Kenya yalikuwa yanajitayarisha kufanya mashambulizi mapya kuuchukuwa mji muhimu kusini mwa Somalia, hata baada ya Rais Ahmed kutokubali operesheni hizo za Kenya.

Othman Miraji amezungumza na mwandishi wa Deutsche Welle huko Mogadishu, Hussein Aweis, kuhusiana na mabadiliko haya ya ghafla kutoka upande wa serikali ya Somalia.

Mahojiano: Othman Miraji/Hussein Aweis
Mhariri: Maryam Abdalla