Somalia yakata uhusiano na Guinea
5 Julai 2019Matangazo
Wizara ya mambo ya nje ya Somalia mjini Mogadishu imesema Jamhuri ya Somaliland ilijitangazia uhuru wake mnamo mwaka 1991 lakini haitambuliki kimataifa na hivyo inachukuliwa tu kama eneo la Somalia lililojitenga.
Wizara hiyo inasema Somalia imekata mahusiano ya kidiplomasia kutokana na Guinea kumpokea kiongozi wa Somaliland na kumpa heshima ya rais wa nchi.
Somalia imeilaumu Guinea kwa kupuuza maazimio na makubaliano yote ya Umoja wa Nchi za Afrika.
Bihi na ujumbe wake walikutana na maafisa wa Guinea na walijadili juu ya kuanzisha uhusiano kati ya Somaliland na Guinea, lakini serikali ya jimbo la Somaliland haijasema chochote juu ya ziara hiyo ya kiongozi wake.