1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yahitaji misaada zaidi.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CWJL

Mogadishu. Afisa wa umoja wa mataifa anayehusika na misaada ametoa wito leo wa kupatiwa misaada zaidi kwa nchi ya Somalia , ambako watu 6,000 wameuwawa katika mapigano mwaka huu. John Holmes akiwa katika ziara nchini Somalia , alikuwa anatarajiwa kumshinikiza rais Abdullahi Yusuf na waziri mkuu mpya Nur Hassan Hussein kuweza kupata msaada wao kupeleka misaada kwa maelfu ya Wasomalia waliondolewa katika makaazi yao kutokana na mapigano baina ya majeshi ya serikali yanayoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia kwa upande mmoja na wapiganaji wa Kiislamu. Wakati huo huo waziri mkuu mpya wa Somalia Nur Hassan Hussein amelitaja baraza lake la mawaziri lenye kujumuisha pande zote katika mzozo wa nchi hiyo jana na kutoa wito wa mazungumzo na wapinzani ili kumaliza mapigano dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu.