Somalia: Rais atia saini sheria ya kurefusha muda wake
14 Aprili 2021Matangazo
Mvutano huo unaongeza mgogoro wa kisiasa wa miezi kadhaa baada ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari kucheleweshwa. Wakosoaji wanasema muda wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed kusalia madarakani umemalizika.
Jamii ya kimataifa ilipinga sheria hiyo ya Rais Mohamed kuendelea kusalia madarakani, na imeonya kuwa kundi la kigaidi la Al-Shabab huenda likatumia mwanya huo wa mgawanyiko wa kisiasa kufanya mashambulizi.
soma zaidi: UN yawahimiza viongozi Somalia kuafikiana juu ya uchaguzi
Jana Jumanne, Rais huyo alitia saini sheria tata baada ya bunge nchini humo mapema wiki hii kupiga kura ya kuendelea kusalia madarakani kwa miaka miwili zaidi.
Hata hivyo, viongozi wa baraza la Seneti la nchi hiyo wamesema kura hiyo haramu.